September 29, 2019


Meddie Kagere, kiongozi wa safu ya ushambuliaji ndani ya Simba amevunja rekodi yake aliyoweka msimu uliopita ndani ya ligi kuu kwenye mechi tatu za mwanzo ambazo ni sawa na dakika 270 kwa kufunga mabao nane ambayo ni mengi kuliko msimu uliopita.

Msimu wa 2018/19 Simba kwenye michezo mitatu ya awali ya ligi kuu ilifunga jumla ya mabao matatu ndani ya dk 270 na yote yalifungwa na Kagere ambapo ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons 1-0, Simba 2-0 Mbeya City (mechi zote Uwanja wa Taifa) na ule dhidi ya Ndanda Uwanja wa Nangwanda Sijaona ilitoka suluhu.

Rekodi ya Simba imevunjwa kwa kuwa msimu huu wa mwaka 2019/20 ndani ya michezo mitatu wamefunga jumla ya mabao nane huku Kagere akifunga matano mengine mawili yakifungwa na Miraj Athuman na lingine na nahodha msaidizi Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

Kagere pia amehusika kwenye jumla ya pasi mbili za mwisho ambapo alitoa kwa Miraji Athuman kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania na Mohamed Hussein kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar tofauti na msimu culiopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic