STRAIKA AWAKIMBIZA MASTAA SIMBA
Imezoeleka kwamba mastaa wa nje ambao wanacheza ligi kubwa zile za Ulaya ndiyo ambao wanaongoza kwa kumiliki magari makali ambapo ushindani kwelikweli kutoa gharama kubwa katika kuyanunua.
Lakini hivi ushawahi kujiuliza kwa hapa nchini katika vikosi viwili vya Simba na Yanga ni nani ambaye anatisha kwa kumiliki gari kali na la thamani kubwa zaidi kuliko wachezaji wote? Kama bado hujafahamu chukua juisi yako kisha kaa chini vizuri ili ufahamu nani ambaye anakimbiza.
Kwa uchunguzi ambao umefanywa na Championi Jumamosi ni kuwa nahodha wa Simba, John Bocco ndiye ambaye anakimbiza katika mastaa wa Bongo ambao wanamiliki mkoko wenye thamani kubwa zaidi.
Bocco ambaye kwa sasa anashuhudia mechi za klabu yake kideoni kutokana na majeraha anamiliki ndinga aina ya Toyota Harrier ambalo ndilo gari kali na la thamani zaidi kama utawachukua mastaa wa Simba na Yanga.
Bocco aliyetua Simba misimu miwili nyuma akitokea Azam FC anamiliki gari hilo ambalo kwa mujibu wa watu wanaohusika na magari wanataja linauzwa kuanzia shilingi milioni 30 na mwisho wake ni shilingi milioni 28 ambao ni usajili wa mchezaji Ally Sonso wa Yanga na chenji inabaki.
Ndinga hilo ambalo humgharimu Bocco fedha nyingi alinunua wakati ambao alisajiliwa na Simba kwa mara ya kwanza wakati akitokea Azam FC ambapo amekuwa akitinga nalo kwenye mazoezi ya timu hiyo kwenye viwanja mbalimbali.
Bocco anawakimbiza mastaa hao kwa gari kutokana na wengi kumiliki magari aina ya Crown ambalo thamani yake sokoni ni Sh milioni 15.
Wachezaji ambao wanatumia usafiri huo ni pamoja na Ibrahim Ajibu, Hassan Dilunga, Gadiel Michael na Jonas Mkude ambao wenyewe wanatumia gari hilo wakiwa sambamba na kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera.
Baadhi ya mastaa wa Yanga ambao wanamiliki mikoko ni Kelvin Yondani anayemiliki Pajero Mini la Sh milioni 14 huku Ramadhan Kabwili anayetembelea Toyota Brevis ambalo hadi unalitia mkononi lazima Sh milioni 12 ikutoke.
Lakini kuonyesha kwamba ndinga hilo la Bocco siyo la mchezo kupata tairi moja tu ni lazima utoe kitita cha Sh 150,000 ambapo kwa tairi zote nne straika huyo akitaka kuzibadili basi lazima aache laki 600,000.
Ndinga hilo linamlia fedha kweli mshambuliaji huyo kwani kupata taa tu nako mziki wake siyo wa kitoto kwani taa mbili za mbele tu ni Sh 300,000 wakati zile za nyuma zote mbili ni Sh 250,000.
0 COMMENTS:
Post a Comment