September 19, 2019


MARK Schwarzer kipa wa zamani wa Chelsea amesema kuwa mlinda mlango namba moja wa Manchester United, David de Gea amekuwa akionyesha uwezo wa kawaida tofauti na zamani.

De Gea ambaye amesaini mkataba mpya ndani ya United utakaodumu mpaka 2023 amekuwa akibebeshwa lawama kwa kufanya makosa yanayoifanya timu yake kufungwa.

Alikubali kufungwa kiulaini kwenye michezo ya Ligi Kuu England wakati United ilipocheza dhidi ya Crystal Palace na Southampton.


Schwarzer amesema kuwa mabao mengi anayofungwa yanatokana na makosa yake binafsi.

 "Mabao mengi anayofungwa yametokana na makosa yake binafsi, makosa aliyofanya kipindi hicho ni mengi kuliko aliyofanya miaka sita au saba, iliyopita," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic