Aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi wa klabu ya simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa kwa sasa hataki tena kuendelea na kazi hiyo sababu ya siasa za mpira wa Tanzania.
Julio ambaye mara ya mwisho aliifundisha Dodoma FC ya jijini Dodoma, amesema ameamua kupumzika zaidi kwanza na atakapokuwa tayari atarejea tena kazini.
Kauli hiyo imekuja akieleza soka la Tanzania limekuwa na siasa nyingi ikiwemo mipango ya upangaji wa matokeo haswa katika timu za daraja la kwanza sambamba na Ligi Kuu bara.
Amefunguka kwa kusema ifikie hatua soka la Tanzania linapaswa kubadilika akieleza timu ndogo za daraja la kwanza zinapambana lakini mwisho wa siku zinaangushwa na baadhi ya watu waiso na mema ndnai ya soka la Tanzania.
"Unajua soka letu lina mipango mingi jambo limepelekea mimi kuamua kupumzika kwa muda kufundisha soka.
"Siasa hizi hazinipi nafasi tena ya kufundisha na badala yake nimeamua kupumzika mpaka nitakapopata tena muda siku nyingine nitaamua kurejea kwenye nafasi hiyo."
Pole sana kaka unatakiwa uendane na mazingira yalivyo ndio ulivyo mpira wa Bongo hakuna maendeleo yeyote brabra nyingi mno
ReplyDelete