September 18, 2019


Mjumbe wa Baraza la Wazee katika klabu ya Yanga, ameibuka na kusema uongozi wa timu yake kuna maagizo aliwapa ili washinde mechi dhidi ya Zesco United lakini hawayakuyatekeleza.

Yanga Jumamosi iliyopita ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhdi ya miamba hao wa Ndola, Zambia katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akilimali ameibuka na kueleza kuwa kuna mambo aliwaambia mabosi wa timu hiyo lakini hawakuweza kumsikiliza na mwisho wa siku matokeo yakawa sivyo.

Akilimali amefunguka kuwa kuna mipango mtu wake maalum alikuwa ameshaiandaa ili Yanga ipate matokeo lakini mawasiliano na uongozi yakawa ndivyo sivyo.

"Ujue Yanga hawakutaka kufanya kile ambacho niliwaambia, kuna mipangp tayari ambayo mimi nilikuwa nimeshaiandaa.

"Tumeshindwa kupata matokeo nyumbani na imenisikitisha zaidi, siwezi kuliongelea sana ila wameniangusha."


3 COMMENTS:

  1. NAWASIHI WANAYANGA MUWE NA UMOJA NA MSHIKAMANO NA MYAPUUZE HAYA MADAI

    ReplyDelete
  2. Hii blog inaamini uchawi katika soka kama Hanna cha kuandika acheni tu tafadhali muwe mnapima vitu kabla ya kuanfuka

    ReplyDelete
  3. jamani labda ni mipango ya kuonga marefa nyie mmejuaje kama ni uchawi mnaona nyie umewajaa kichwani?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic