September 28, 2019



ZDRAVCO Logarusic, aliyekuwa Kocha wa  Simba zamani kwa sasa anaifundisha timu ya Taifa ya Sudan amesema kuwa Azam FC na Yanga zina deni kubwa kwa Taifa la Tanzania ambalo uwezo wa kulilipa lipo miguuni mwa wachezaji endapo wataacha papara wakiwa kwenye lango.

Azam na Yanga, leo zinashuka uwanjani ambapo Yanga inapeperusha bendera kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na itamenyana na Zesco United huku Azam FC ikiwakilisha Taifa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika itamenyana na Triangel United.

Akizungumza na Saleh Jembe, Logarusic amesema kuwa aliutazama mchezo wa kwanza wa Yanga dhidi ya Zesco na kuona namna ilivyolazimisha sare ya kufungana bao 1-1 huku Azam FC ikipoteza mbele ya Triangle United ya Zimbabwe kwa kufungwa bao 1-0.

"Nimeona namna Yanga inavyocheza pamoja na wapinzani wao walivyo si timu ya kubeza Zesco ipo fiti, hata Azam pia bado wapinzani wao ni wagumu ila wanafungika iwapo wachezaji hasa safu ya ushambuliaji Ikipunguza papara.

"Tanzania kuna vipaji na wachezaji wengi wanajisahau wakiwa uwanjani, kwa upande wa wakilishi wa Tanzania Yanga na Azam wana kazi kurejesha furaha na kufunga mabao mengi ya mapema inawezekana wakiamua," amesema.

Timu mbili ili kusonga hatua inayofuata ni lazima zishinde, ikitokea zikakwama Azam itakuwa imefungashiwa virago jumla huku Yanga akidondokea kwenye Kombe la Shirikisho.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic