September 28, 2019





Mtibwa Sugar imecheza jumla ya michezo minne na imeambulia pointi moja pekee baada ya kutoa sare na JKT Tanzania huku ikachapwa na Lipuli, Simba na Tanzania Prisons. 

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa matokeo wanayoyapata kwa sasa yanawaumiza kichwa wana imani ya kurejea kwenye ubora wao.

"Tumeshindwa kupata matokeo mazuri kwenye michezo yetu ya mwanzo hii ni changamoto mpya ambayo inatupa taabu kwa sasa, ila niwaambie mashabiki kwamba bado ligi inaendelea tutafanya vizuri," amesema Kifaru.

Kesho Mtibwa Sugar itaikaribisha Mbeya City uwanja wa Jamhuri kwenye mchezo wao wa ligi.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic