LEO timu ya
Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itakuwa kazini kumenyana na timu ya Burundi
kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar
wamepewa tahadhari na Kocha wa zamani wa Simba na Dodoma FC, Jamhuri Khiwelo
‘Julio’.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Julio amesema kuwa wachezaji wanapaswa kuingia uwanjani wakiwa na
nidhamu kwa wapinzani wao kwani wakiwadharau wataambulia maumivu.
“Wachezaji jukumu lao kutambua kwamba wapinzani wao wanahitaji pia ushindi ndio maana
wamekuja nchini, kazi kubwa inayotakiwa ni kujituma na kupata ushindi wa mapema
ili kujiongezea nafasi ya kujiamini.
“Makosa
mengi yamekuwa ni kwa upande wa umaliziaji wa nafasi zinazotengenezwa kwa kuwa
tutakuwa nyumbani basi mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu ya
Taifa,” amesema.
Mchezo wa
kwanza nchini Burundi, Stars iliyo chini ya Kaimu Kocha Etienne Ndayiragije
ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 leo inakazi ya kutafuta ushindi kusonga
mbele hatua ya makundi.
Kocha wa Simba??Patrick Aussems. Julio ni kocha aliyefukuzwa Dodoma.Lwandamina nae ni kocha wa Yanga!!!Acheni ujinga. Wekeni vichwa vya habari vinavyoendana na habari yenyewe.
ReplyDelete