September 14, 2019


FULL TIME; YANGA 1-1 ZESCO UNITED
Dak ya 90+4 Kamusokooooooo, anaisawazishia Zesco dakika za usiku kabisa, sasa ni 1-1.
Dak ya 90, sasa zimeongezwa dakika nne.
Dak ya 90, anapiga lakini inawababatiza wachezaji wa Zesco.
Dak ya 89, yanga wanapata faulo nje kidogo ya 18, anapiga Sibomana, akionesha utulivu anaweza akafunga bao la pili, ngoja tuone.
Dak ya 83, wanachokifanya Yanga ni kulinda zaidi lango lao kwa sasa.
Dak ya 80, zimesalia dakika 10 pekee mpira kumalizika

Dak ya 75, Zesco wanapata nafasi ya kuandika bao nao wanashindwa kuhimili umaridadi wa Mnata.
Dak ya 75, Kalengo anapata nafasi nzuri lakini anakosa utulivu wa kufunga bao la pili kwa Yanga.
Dak ya 74, Yanga wanafanya mabadiliko, anaingia Ali Ali kuchukua nafasi ya Mapinduzi Balama
Dak ya 64, ni faulo kwa Yanga, eneo la pembeni nje kidogo ya 18 kulia mwa uwanja, imepiga lakini Zesco wanaokoa
Dak ya 61, Zesco wanapiga lakini inakuwa faulo, faida kwa Yanga.
Dak ya 60, Zesco wanapata kona

Dak ya 58, Urikhob anatoka kuchukua nafasi ya Maybin Kalengo, wakati huo Banka anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Ngassa.
Dak ya 56, kila timu inaonesha jitihada za kuweka kambani bao la pili.
Dak ya 53, Hatariiii, Tshishimbi anakosa nafasi akiwa yeye na kipa, anapiga kichwa ambacho kinaenda kushoto mwa lango la Zesco United.
Dak ya 50, Yanga wanamilki mpira tena, anao Balama, bado Yanga wanaendelea kusaka bao la pili, mpira unamkuta Feisal Toto.

Dak ya 49, Kona ya tatu Zesco wanapata kwa kipindi hiki cha pili.
Dak ya 48, Mnata anafanya maajabu ya kusevu nafasi nyingine akiokoa shambulizi la Zesco.
Dak ya 48, Sibomana anafanya jaribio lingine lakini linashindwa kuza matunda
Dak ya 47, Balama anapoteza nafasi, Zesco wanachukua mpira.
Dakika 45 za kipindi cha pili zimeanza

MAPUMZIKO: YANGA 1-0 ZESCO UNITED
Dak ya 45, Banka anapewa kadi ya njano kwa kucheza madhambi dhidi ya mchezaji wa Zesco, dakika moja imeongezwa kuelekea mapumziko.

Dak ya 43, kwa namna timu zote mbili zinavyocheza kila mmoja ana uwezo wa kupata matokeo licha Yanga kuwa inaongoza.
Dak ya 42, jaribio jingine wanalipata yanga lakini mawasiliano ya yanakuwa si mazuri, wanashindwa kulitumia.
Dak ya 37, Zesco wanafanya mabadiliko, anaingia Wiston Kalengo na anatoka Enock.
Dak ya 32, Zesco wanaonekana kutulia zaidi kwa sasa wakisaka bao la kusawazisha, wanajaribu kutafuta nafasi ya kufunga bao.
Dak ya 29, Yanga wanazidi kupata moto sasa, wanashambulia lango la Zesco kama nyuki.
Dak ya 24, Gooooooli, Sibomana anafunga penati yake kwa umaridadi kabisa, sasa Yanga wako mbele kwa bao 1-0.
Dak ya 23, penatiiiii, Yanga wanapata penati baada ya Sibomana kufanyiwa madhambi eneo la hatari, ni faida kwa Yanga. Anaenda kupiga Sibomana mwenyewe.

Dak ya 21, kosakosa nyingine imetokea kwenye lango la Zesco, inakuwa faulo na Mwamuzi anaamuru mpira upigwe kuelekea Yanga.
Dak 20, Zesco wanaonekana kutawala zaidi eneo la kati wakiwazidi Yanga japo kuipenya ngome ya wapinzani wao imekuwa ngumu.
Dak ya 19, Mpira unatoka nje na unakuwa wa kurushwa kuelekezwa lango la Zesco, tayari usharushwa.
Dak ya 18, Mnata anakuwa shujaa kwa mara nyingine tena, anaokoa shuti ambalo lingeweza kuwa msala kwake na Yanga.
Dak ya 15, Sibomanaaaaaa, anapiga kichwa kufuatia krosi safi ya Tshishimbi lakini inakwenda nje, ilikuwa nafasi nzuri sana kwa Yanga kaundika bao.

Dak ya 14, Zesco wanapata kona ya kwanza, wanapiga na inaleta hatari pale, Mnata anadaka, wanaanza upya.
Dak ya 11, Balamaaa anapiga shuti moja kaliii lakini linakwenda sentimita chache kulia kushoto mwa lango la Zesco.
Dak ya 10, Mnata anadaka mpira mwingine uliotokana na shambulizi kutoka kwa Zesco, kushoto mwa Uwanja.
Dak ya 7, shambulizi jingine wanafanya Zesco lakini uimara wa Mnata unasaidia, anaanzisha upya.
Dak ya 6, Fei Toto naye anapata nafasi ya kujaribu kufunga lakini anapiga mpira nje, ni golikiki.

Dak ya 5, Kamusoko anapata nafasi na anapiga shuti kali lakini uimara wa Mnata unamfanya adake kwa umaridaidi kabisa.
Dak ya 5, Mnatana anaonekana akipaza sauti kuwahamasisha wachezaji wenzake ndani ya uwanja wapambane.
Dak ya 4, Yanga wanajaribu shambulizi la kwanza ambalo linamfikia kipa wa Zesco na wao wanaanza upya.
Dak ya 3, Balama anatuliza  mpira kulia mwa uwanja, nyuma kidogo ya lango lake, anapia pasi kwenda mbele.
Dak ya 1, tayari mechi imeshaanza katika uwanja wa Taifa.

2 COMMENTS:

  1. Kwa timu zenye Uzoefu wa CAF mfano TP Mazembe, Zesco, Al Ahly na Esperance usitegemee hizo timu hazitajipanga na kutumia uwanja wao wa nyumbani vizuri...........Kocha kashawateka na kuziiba akili za wanayanga....itachukua muda kumgundua.....Tatizo sio wachezaji tatizo ni mbinu walizofundishwa ili wafunge magoli....hili ndio tatizo. Forward ya Yanga ni nzuri ila tatizo ni namna wanavyofundishwa ili wapate mabao hiyo ndio shida.....ukitaka kujua mpeni Patrick Aussems forward hii hii uone kama hawatafunga?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic