BAHARIA KAMUSOKO AIPA MLIMA YANGA MECHI IKIMALIZIKA KWA SARE YA 1-1
Timu ya Yanga imeanza kwa sare ya 1-1 dhidi ya Zesco United katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo iliyokuwa ya hatua ya kwanza katika mashindano hayo, imeshuhudiwa na idadi hafifu ya mashabiki waliojitokeza kuipa sapoti Yanga.
Bao la kwanza katika mchezo huo limewekwa kimiani kupitia kwa Patrick Sibomana aliyefunga mnamo dakika ya 24 kwa njia ya penati baada ya kufanyiwa madhambi eneo la hatari.
Bao hilo lilidumu kwa dakika 45 za kwanza mpaka ilipowachukua Zesco kusawazisha dakika za jioni kabisa kupitia kwa Thaban Kamusoko akipiga shuti kali lililomshinda kipa Metacha Mnata.
Yanga itakuwa tena na kibarua kingine katika mchezo wa marudiano utakaochezwa jijini Ndola, Zambia Septemba 27, na ili isonge mbele inapaswa kuibuka na ushindi wa aina yoyote.
Kwa timu zenye Uzoefu wa CAF mfano TP Mazembe, Zesco, Al Ahly na Esperance usitegemee hizo timu hazitajipanga na kutumia uwanja wao wa nyumbani vizuri...........Kocha kashawateka na kuziiba akili za wanayanga....itachukua muda kumgundua.....Tatizo sio wachezaji tatizo ni mbinu walizofundishwa ili wafunge magoli....hili ndio tatizo. Forward ya Yanga ni nzuri ila tatizo ni namna wanavyofundishwa ili wapate mabao hiyo ndio shida.....ukitaka kujua mpeni Patrick Aussems forward hii hii uone kama hawatafunga?
ReplyDeleteumesema kweli kabisa. yaani kwa mechi ya jana yanga alipaswa afunge goli tatu, nakosa lilifanyika alipotoka banka, alikuwa anakata umeme wa wale jamaa akishirikiana na tshishimbi na toto. sasa alipotoka akaingia kalengo na game ilianza kuwa ngumu ikamshinda akawa anaanguka hovyo.
Deletekocha ni tatizo pale yanga, na mkiti wao amelijua,beki za yanga pia ni shida,bado hakuna pacha nzur kati ya yondan na ally ally,kocha maneno mengi vitendo 0