September 15, 2019



MENEJA wa Norwich, Daniel Farke amesema kuwa wakati mwingine ubora wa kikosi cha Manchester City huwa kwenye ubora kiasi kwamba hauwezi kuwafunga kirahisi.
Norwich iliinyoosha Manchester City kwa mabao 3-2 mchezo wa Ligi Kuu England jambo lililowafanya wengi kushangazwa na maajabu ya kikosi hicho huku moto wa Teemu Pukki ukiwa wa hali ya juu kwani alifunga bao moja na kutoa pasi ya bao.
"Muda mwingine ubora wa kikosi cha Manchester City, hauwezi kukifunga kutokana na ubora wake ulivyo, sioni kama nimefanya jambo kubwa sana ila napongeza morali ya wachezaji wangu," amesema.
Meneja wa Man City, Pep Guardiola amesema kuwa hana mashaka na kupoteza pointi tatu kwani muda bado upo.
"Kwa sasa hakuna cha kuhofia bado tupo Septemba unadhani kuna bingwa atatangazwa muda huu? Bado kazi inaendelea na nitaongea na wachezaji wangu," amesema. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic