September 15, 2019


OFISA Habari wa michuano ya Sprite B Ball Kings, Goza Chuma amesema kuwa mashabiki wasiache kujitokeza kwa wingi uwanja wa ndani wa Taifa kushuhudia burudani za fainali za michuano hiyo ambayo kwa sasa ipo hatua ya robo fainali.

Akizungumza na Saleh Jembe, Chuma amemsema kuwa ushindani msimu huu ni mkubwa na kila timu inahitaji kupata ushindi jambo linalonogesha mashindano hayo.

"Robo fainali ni ngumu na kila timu inatafuta ushindi kwani timu awali zilikuwa 60 zimechujwa mpaka tukafika na timu 16 kabla ya kupata nane ambazo zimetinga robo fainali.

"Cha msingi tu niwaambe mashabiki ni muda wa kujitokeza kuona namna ushindani ulivyo kila timu inapambana na hakuna kiingilio," amesema.

Huu ni msimu wa tatu wa michuano hii ya B Ball Kings huku bingwa wa muda wote akiwa ni Mchenga B Ball.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic