PATRICK Aussems, raia wa Ubelgij Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wanatambua kikosi cha Mtibwa Sugar sio cha kubeza kutokana na ubora ila wao lengo lao ni moja tu kupata ushindi.
Simba itashuka uwanja wa Uhuru Septemba 13 kumenyana na Mtibwa Sugar ikiwa ni mchezo wake wa pili wa ligi baada ya ule wa kwanza kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya JKT Tanzania.
Akizungumza na Saleh Jembe, Aussems amesema kuwa maandalizi ya kikosi yapo vizuri na kila mchezaji anajua jukumu lake la kufanya kuelekea mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar.
"Tunahitaji kufanya vizuri na kupata matokeo mbele ya Mtibwa Sugar, kikubwa ambacho kwa sasa tunakifanya ni kumalizia maandalizi ya mwisho kabla ya kukutana nao uwanjani.
"Ushindani ni mkubwa kwani kila timu inahitaji ushindi tumejipanga kufanya vema sapoti tunahitaji kutoka kwa mashabiki," amesema.
Simba ni mabingwa watetezi wa ligi, mchezo wao wa mwisho msimu uliopita walishinda kwa idadi ya mabao 3-0 mbele ya Mtibwa uwanja wa Uhuru leo wamefanya mazoezi viwanja vya Gymkyana.
0 COMMENTS:
Post a Comment