September 29, 2019


KELVIN John na Andrew Simchimba washambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya miaka 20 leo wameuwasha moto kwenye mchezo dhidi ya Uganda ambao ni wa hatua ya robo fainali michuano ya Cecafa kwa kutimiza majukumu ya Taifa kisawasawa.

Tanzania imeshinda jumla ya mabao 4-2 kwenye mchezo wa leo dhidi ya wenyeji Uganda na kuifanya itinge moja kwa moja hatua ya nusu fainali.

Tanzania ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya 25 na bao la pili dakika ya 60 kupitia kwa Simchimba huku Kelvin John akipachika mabao yake dakika ya 88 na 90 na yale ya Uganda yakipachikwa na Abdul Aziz.

Washambuliaji hao wote kwa sasa wametupia kambani jumla ya mabao sita na kila mmoja ana hat trick moja mguuni mpaka sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic