UWANJA WA SIMBA BUNJU WAKARIBIA KUTUMIA, VYUMBA VYA KUBADILISHIA NGUO HATUA YA MWISHO
Ujenzi wa uwanja wa klabu ya Simba uliopo huko Bunju, jijini Dar es Salaam unazidi kushika kasi.
Kutokana na kasi ya ujenzi wa uwanja huo hivi sasa, inaelezwa kuna uwezekano ndani ya wiki chache zijazo Simba wanaweza wakaanza kuutumia haswa ule wa nyasi asili.
Mbali na nyasi asili kuota, inaelezwa pia harakati za kuanza utandazaji wa kapeti kwa uwanja mwingine utaanza pia hivi karibuni.
Wakati huohuo taarifa zinasema vyumba vya kubadilishia nguo ndani ya uwanja huo vinaelekea kukamilika hivyo kwa namna moja ama nyingine inaashiria unaweza kuanza kutumika.
Simba ikikamilisha ujenzi wa uwanja huo itakuwa imeandika historia dhidi ya watani zao wa jadi Yanga kwa kuwa na uwanja wake wa mazoezi ambao timu hizo hazikuwa nao kwa zaidi ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.
Simba ndio hawajawa na uwanja kwa zaidi ya miaka 80,Yanga walishtakiwa nao
ReplyDelete