RAIS TFF ATOA UFAFANUZI WA KAPOMBE KUTEMWA STARS
Na George Mganga
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ametolea ufafanuzi wa suala la mchezaji wa Simba, Shomari Kapombe, kuondolewa katika timu ya Taifa.
Akizungumza na Radio TK FM ya jijini Tanga, Karia amesema Kapombe aliondolewa baada ya kuomba ruhusa kuwa hali yake si nzuri kiafya.
Kauli hiyo imekuja kufuatia sintofahamu juu ya mchezaji huyo wengi kuhoji kwanini hajajumuishwa ndani ya kikosi hicho licha ya kupata namba ndani ya klabu yake.
"Shomari Kapombe alimuomba mwenyewe Mwalimu wa timu ya Taifa ya kuwa bado hajapona vizuri.
"Akamuomba apumzike kucheza na kweli kocha amemuacha mpaka awe fiti na akija kuona tena baadaye anafaa atamuita," alisema Karia.
0 COMMENTS:
Post a Comment