UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa haujafurahishwa na matokeo mabovu uliyoyapata hivi karibuni kwenye michezo ya awali ya Ligi Kuu Bara unapasua kichwa kupata dawa ya kuondoa balaa hilo.
Mtibwa Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu, Zuber Katwila imepoteza michezo yake yote miwili iliyocheza ikiwa ugenini kwa kuanza kupokea kichapo mbele ya Lipuli kwa kufungwa mabao 3-1 kabla ya kupoteza mchezo wa pili mbele ya Simba kwa kufungwa mabao 2-1.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wameumizwa na matokeo mabavu waliyoyapata kwa sasa wanayafanyia kazi makosa yao.
"Tumeboronga vibaya michezo yetu ya mwanzo ni picha mbaya na mwanzo mbaya ila hakuna namna kwa kuwa ni matokeo tuna jipanga kufanya vema michezo yetu inayofuata.
"Kwa sasa kikosi kipo makao makuu Morogoro na hesabu zetu ni kurejea kwenye ubora hivyo ni suala la muda tu kazi itaanza kuonekana uwanjani, dawa ya kupata matokeo mazuri tumeshaijua na mapungufu yetu tumeyajua" amesema.
Kwenye michezo miwili, Mtibwa Sugar imefungwa jumla ya mabao matano na imefunga jumla ya mabao mawili.
0 COMMENTS:
Post a Comment