September 16, 2019


WINGA wa Crystal Palace, Wilfried Zaha amempiga chini mazima wakala wake kwa kushindwa kufanikisha dili lake la kusepa klabuni hapo.

Kabla ya kuanza kwa msimu huu, Zaha alikiri kuwa alikuwa tayari kutafuta changamoto mpya Ulaya na alikuwa anapigiwa hesabu na Arsenal pamoja na Everton.

Dili la kusepa kwake lilibuma baada ya klabu yake kuweka dau la pauni milioni 80 (sh bilioni 226) kwa klabu yoyote ambayo ilitaka kumsajili jambo lililokuwa zito.

Imeelezwa kuwa Zaha alimwambia wakala wake huyo, Will Salthouse kuhusu mipango yake lakini ikashindikana na ndipo akamruhusu asepe.


Kwa sasa Zaha ameamua kuweka habari za kusepa pembeni na kupambana ndani ya kikosi chake kufanya maajabu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic