September 30, 2019


Ni kama mtihani mzito kwa Mshambuliaji wa Yanga, David Molinga 'Falcao' aliyetakiwa na Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kufunga mabao zaidi ya ishirini msimu huu, hii ni baada ya Meddie Kagere kuingia tena kambani.

Jana Simba ilifanikiwa kuifunga Biashara United katika mchezo wa ligi kuu huku Kagere akifikisha jumla ya mabao sita ndani ya mechi nne alizocheza.

Idadi hiyo ya mabao inakuwa inamuumiza Falcao namna ya kufukuzana na Kagere kwani timu yake imeshacheza mchezo mmoja pekee wa ligi na ikipoteza uliokuwa dhidi ya Ruvu Shooting.

Mbali na Falcao kuwa na mzigo huo dhidi ya Kagere, inawezekana pia Zahera akawa anaumiza kichwa kwa namna ya kumuweka sawa kisaikolojia mchezaji wake kwani kufikisha mabao 20 kwa Falcao si mchezo.

4 COMMENTS:

  1. Ahadi ya Zahera ni kuwa kama mchezaji huyo hajafunga mabao ishirini akatwe mkono. Ahadi nyengine ni mbaya na hatati kwani huyo ni binaadamh na kufanikiwa na kutofanikiwa ni mikononi mwa Mungu

    ReplyDelete
  2. Hapo Hamna Straika Ni Bora Yule Makame Akicheza Mbele Yupo Vizuri Sana Na Washauri Simba Tumsajili Dilisha Dogo Achukue Nafasi Ya Okwi Maana Mashine Aliyo Iachia Kwa Golikipa Wake Linaonyesha Jinsi Ilivyo Mahili Ktk Sekta Ya Ufunguji

    ReplyDelete
  3. Nakuunga mkono. Makame ni bonge la straika .Goli lake ni mojawapo ya magoli bora msimu huu kwenye mashindano ya CAF.Ilikuwa bonge ya bunduki.

    ReplyDelete
  4. Makame alitokea Simba akarudi kwai Zanzibar kabla ya kusajiliwa Yanga
    Itakuwa vizuri Simba wakimsajili tena
    Kessy kabla ya kuandika Simba alianza Vituko mara faul sa penalty mara kujitafutia red card...yani chochote chan kuigharimu tumu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic