September 19, 2019


Baada ya washambuliaji wa Yanga kushindwa kufanya vizuri kwenye mchezo uliopita dhidi ya Zesco, hatimaye kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera ameamua kubadili programu yake ya mazoezi.

Yanga walitoka sare ya bao 1-1 na Zesco ya Zambia kwenye mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi iliyopita, lakini washambuliaji wa timu hiyo walikosa nafasi nyingi.

Yanga imefanya usajili kabambe msimu huu ambapo imewasajili washambuliaji Juma Balinya, Patrick Sibomana, Issa Bigirimana na Sadney Urikhob lakini wote wameshindwa kuwika.

Chanzo cha ndani kutoka Yanga kimesema kuwa sasa Zahera amekuwa akifanya mazoezi na mchezaji mmojammoja badala ya kundi kama ilivyokuwa awali. “Kocha kuanzia mchezo ule umalizike amekuwa akidili na mchezaji mmojammoja, hataki tena kudili na kundi, anamfundisha Balinya mwenyewe, baadaye Sibomana na wengine.

“Anaamini hii itakuwa njia pekee ya kuweza kupata mafanikio kwenye mchezo wa pili,” kilisema chanzo. Hata hivyo, akizungumza na Championi Jumatano, kuhusiana na ishu hiyo, Zahera amesema kuwa programu hizo tayari kila mshambuliaji ameshaanza kuzifanyika kazi hivyo anaamini katika mchezo wa marudiano mambo yatakuwa sawa.

“Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu ya mchezo wa marudiano dhidi ya Zesco ambao tutacheza hivi karibuni huko Zambia. “Upungufu wote uliojitokeza katika mchezo wa kwanza tuliocheza hapa Dar es Salaam, nimeshaufanyia
kazi na zaidi ni katika nafasi ya ushambuliaji.

“Kuna programu maalumu ambazo nimewapa washambuliaji wote kabla ya mchezo wa marudiano, lengo likiwa ni kuhakikisha wanakuwa fiti lakini pia wepesi katika kuzitumia vizuri nafasi za kufunga watakazokuwa wakizipata,” alisema Zahera.

2 COMMENTS:

  1. Zesco 2 Yanga 0 mechi ya marudiano Ndola September 28, 2019

    ReplyDelete
  2. Al umekazania hayo matokeo kinoma....au umebet! Anyway yanga inabidi ijipange kweli kama inataka kupindua meza Ndola! Sjaona chochote kinachoashiria kupata goli kwa open play...lakin wakitafuta set pieces nyingi nyingi wanaweza kupata chochote! Kuumia kwa boxer na mapinduzi balama pia sio habari nzuri sana maana mashambulizi ya Zesco yatakuwa makali mara dufu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic