DANTE ATOA MASHARTI YA MALIPO YA FEDHA ZAKE YANGA, UONGOZI WAMJIBU
Beki wa Yanga, Andrew Vincent 'Dante' amegoma kulipwa kwa mafungu kiasi cha fedha ambazo ni milioni 40 anazoidai klabu yake.
Kwa mujibu wa Ofsa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amesema kuwa mchezaji huyo amegoma na badala yake anataka kulipwa kwa mkupuo.
Bumbuli ameeleza kuwa Yanga ipo tayari kumlipa Dante fedha hizo kwa mafungu akieleza walikuwa wamepanga kuanza kumlipa milioni 15 mara mbili na baadaye watamalizia 10 zitakazobaki.
"Dante anachotakiwa kufahamu ni kuwa si mchezaji pekee anayeidai Yanga, wapo wengi na wote wamekubaliana kulipwa kwa awamu kama ilivyokuwa kwa Juma Abdul ambaye sasa amejunga na timu."
0 COMMENTS:
Post a Comment