October 10, 2019


Mhariri Mtendaji wa Global Publishers na Saleh Jembe, Saleh Ally, amemshauri beki wa kulia wa Smba, Shomari Kapombe kupumzika kwanza ili kuhakikisha anapona kabisa kabla ya kurejea kazini.

Ally ameeleza kuwa ni vema Kapombe akatulia kwanza nje ya uwanja ili apone kabisa, hata kama akichukua msimu mzima akiwa nje ya uwanja ili baadaye akirudi awe fiti.

"Shomari anajua sana, amekuwa na bahati mbaya ya majeruhi.

"Umri bado unameuhusu lakini vizuri ahakikishe amepona kabisa hata kama atakaa nje msimu mzima.

"Majeraha kama unayawahisha kurejea uwanjani inakuwa lahisi kujitonesha na baadaye yanakuwa majeraha ndugu na mwisho unalazimika kustaafu mapema."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic