HEE Chan Hwang, mshambuliaji wa Red Bull Salzburg aliyeishangaza dunia kwa kumpiga chenga beki kisiki wa Liverpool, Virgil Van Dijk asiyepitika kirahisi amesema watapambana kufuzu hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Salzburg ilikonga nyoyo za mashabiki kwa kupiga soka la kiwango licha ya kuambulia kichapo cha mabao 4-3 na Liverpool.
Maajabu ni kwamba timu ilikuwa nyuma kwa mabao 3-0 ngoma ilipinduliwa mpaka kurudisha mzani sawa mwisho ikapigwa 4-3.
Mkorea huyo alianza kufungua ukurasa wa mabao dakika ya 39 alipomlamba chenga Dijk.
"Lengo letu ni kucheza kwenye mtoano, tutapambana bila kuchoka," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment