MCHEZAJI wa
zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania na timu ya Yanga, Sunday Manara ‘Computer’
amefanyiwa upasuaji wa jicho kwenye hospital ya Anglican hivi karibuni na kwa
sasa anaendelea vizuri.
Akizungumza
na Championi Jumatatu, mwanaye Haji Manara ambaye ni Ofisa Habari wa Simba
alisema kuwa ni jambo la kushukuru kwa Mungu kwa mapito wanayopitia na wana
imani kila kitu kitakuwa sawa.
“Kweli baba alikuwa anaumwa na alifanyiwa upasuaji wa jicho pale hospitali ya Anglican ila kwa sasa anaendelea vizuri na amerejea nyumbani baada ya kupatiwa matibabu,” alisema Manara.
Akizungumza na Championi Jumatatu jana jioni, Sunday Manara alisema amkuwa na tatizo la macho kwa muda mrefu na alipokwenda kufanya uchunguzi madaktari wakamshauri afanyiwe upasuaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment