October 7, 2019


Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu (TFF), Michael Wambura ameachiwa huru na mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam.

Wambura ameachiwa huru baada ya kuingia makubaliano na upande wa Jamhuri kulipa zaidi ya TSh milioni 100 ambazo alijipatia isivyo halali.

Ufafanuzi uliotolewa na hakimu mkazi kisutu ni kwamba Wambura atalipa fedha hizo kwa awamu tano na  kwa masharti ya kutofanya makosa yeyote kwa kipindi cha miezi 12, ambapo leo amelipa Tsh milioni 20.

Hii imekuja baada ya Wambura kumuandikia barua Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP)kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alishauri kwa wale wote wenye kesi za uhujumu uchumi kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa yanayomkabili mahakamani hapo.


Awali akiwa mahakamani hapo Wakili wa serikali Wankyo Simon alimsomea shtaka lake moja la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kukiri mbele ya Hakimu wa  mahakama ya Kisutu, Kalven Mhina.

2 COMMENTS:

  1. Kumbe aliiba duuh, majigambo yote hayo kwamba yeye msafi chaliii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahaaaa kumbe kunyanyua mabega kote ni mbwembwee tu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic