October 8, 2019


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema kuwa, mshambuliaji wake, Miraj Athuman maarufu kama Sheva amechukua mikoba ya Emmanuel Okwi katika kuifanya timu hiyo kuendelea kuwa bora kwenye Ligi Kuu Bara.

Kauli ya Aussems raia wa Ubelgiji imekuja ikiwa ni baada ya Sheva aliyejiunga na timu hiyo msimu huu kuanza na moto wa hatari.

Katika mechi nne za Ligi Kuu Bara alizocheza, Sheva amefunga mabao matatu kati ya kumi ambayo yamefungwa na timu hiyo hadi sasa ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 12.

Awali, wakati Okwi anaachana na Simba mwishoni mwa msimu uliopita na kutimkia Misri, ilionekana timu hiyo itayumba, lakini Aussems amesema Sheva ameiweka sawa.

Akizungumzia hilo, Aussems amesema: “Siwezi kuumia kuondoka kwa Okwi kwa kuwa kama mchezaji kuondoka kwenye timu ni jambo la kawaida.

“Ukiangalia hivi sasa, Sheva ameweza kufanikiwa kwa kiasi fulani katika kuifanya Simba iwepo hapa ilipo sasa kutokana na mipango yetu.

“Naamini kama ataendelea kwa kasi na uwezo ambao yupo nao kwa sasa, basi kuna nafasi kubwa ya yeye kufanya vizuri na kuwa mchezaji mkubwa hapo baadaye.”

3 COMMENTS:

  1. Sio sahihi kumfananisha Miraji na Okwi. Tumpe heshima yake Okwi. Miraji anawezakuja kuwa mchezaji mzuri baadae lakini kujidanganya kuwa ameziba pengo la Okwi huko ni kuficha udhaifu wa kushindwa kusajili mchezaji mwenye uwezo sawa ama zaidi ya Okwi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. okwi alikuwaje alivyo kuja simba alichukuwa mda mrefu mpaka kakawa okwi unae mjua lakini huyu miraji amekuja simba mda mfupi na amekuwa mtu muhimu sana simba mimi namyabiria miraji athumani akawa bora kuliko okwi miraji athumani ni wa kiwango cha juu sana na hatokawia simba atakwenda huko aliko samata kwa uwezo wa mwenyeezi mungu pia samata nilimtabiria wakati ule na mungu kasaidi yupo ulaya kwa muono wangu miraji atakuja kuwa bora kuliko samata

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic