October 8, 2019


Mwanamme aitwaye, Isma Ssesanga, wa kijiji cha Kasawa, Wilaya ya Mukono nchini Uganda,  anashikiliwa na vyombo vya dola kwa madai ya kumpiga bintiye hadi kufa kwa kula chakula chake ambacho alikuwa amekiweka kutoka kwenye pati.

Naibu Msemaji wa Polisi wa Kampala, ASP Luke Owoyesigyire, alisema  Ssesanga alianza kuwapiga kwanza watoto wake wawili wa kiume kabla hajamshambulia marehemu, Salama Nassanga, aliyekuwa na umri wa miaka kumi.

Pamoja na Ssesanga kudai kwamba binti huyo alikufa wakati akikimbia kipigo, majirani wamesisitiza kwamba alimshambulia mtoto huyo na kumuua hapohapo.

Imeandaliwa na Global Publishers.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic