FULL TIME: YANGA 3-3 POLISI TANZANIA, MECHI YA LIGI KUU BARA
FULL TIME; YANGA 3-3 POLISI TANZANIA
Dak ya 90, zikiwa zimeongezwa dakika tano, mchezaji mmoja wa Polisi ametolewa nje kwa kupewa kadi nyekundu.
Dak ya 86, Bado timu zote zinapambana kwa ajili ya kusaka matokeo, mashambulizi ya zamu yanaonekana kwa kila uoande.
Dak ya 80, Toto anapewa akdi ya njano, na inakuwa faulo kwenda Yanga, mpira upo kulia mwa uwanja, Polisi wanapiga na mpira unaokolewa.
Dak ya 78, Polisi sasa wkao mbele tena langoni mwa Yanga, Yanga wanaokoa na kupiga mbele.
Dak ya 77, Polisi Tanzania wanapata kona, wanapiga lakini unashindwa kuzaa matunda.
Dak ya 76, mpira umesimama, mchezaji Yanga ameanguka chini.
Dak ya 68, Gooooli, Falcao anaifungia Yanga bao la tatu kwa njia ya faulo.
Dak ya 66, Goooli, Yanga wanapata bao la pili, Molinga anaingia kambani.
Dak ya 63, Polisi wanacheza kwa kujiamini sasa, hawana presha hata kidogo, wakati huo mashabiki hawaamini kinachotokea.
Dak ya 58, Nchimbi tena anafunga bao la tatu kwa njia ya kichwa.
Dak ya 57, Nchimbiiii, anafunga bao la pili kiulaiini baada ya kupokea pasi nzuuri kati mwa uwanja.
Dak ya 54, Kasekeeee, piga shuti kali pale, kipa Kulwa Manzi anadaka kwa umaridadi kabisa.
Dak ya 52, Polisi nao wanakosa nafasi nyingine, inakuwa golikiki.
Dak ya 50, Kosakosa inatokea langoni mwa Polisi, wanatoa nje, ilikuwa ni hatari.
Na mpira ni mapumziko, Yanga 1-1 Polisi Tanzania
Dak ya 45+3, Molinga anakosa kwa kupaisha mpira juu akiwa yeye na mlinda mlango wa Polisi.
Dak ya 45, dakika tatu zimeongezwa kuelekea mapumziko, wakati huo mchezaji wa Polisi yupo chini baada ya kupigwa kiwiko na Moro.
Dak ya 43, bado mpira unachezwa kwa zamu katikati mwa uwanja kwa timu zote mbili.
Dak ya 42, Polisi wanaanza tena upya baada ya Yanga kupoteza mpira, wanasakata mpaka eneo la kati mwa uwanja lakini Yanga wanaunyakua tena.
Dak ya 41, Polisi Tanzania wanashindwa kufunga bao la pili kwa uzembe wao.Dak ya 33, Pigwa pale, goooli, Polisi wanasawazisha kupitia Ditram Nchimbi kwa shuti kali.
Dak ya 32, faulo nyingine inapigwa kwenda Yanga, imepigwa na inakuwa kona.
Dak ya 32, Offside, Abdul anaotea, mpira unaelekezwa Yanga.
Dak ya 30, Juma Abdul anaruhusu mpira unatoka kizembe, Polisi wanaenda kurusha.
Dak ya 29, Polisi wanapiga, inakwenda juu ya lango.
Dak ya 28, Mnata anaonekana na mpira, anatoa maelekezo kwa wachezaji wake, anapewa kadi ya njao baada ya kuushika mpira nje ya eneo lake, na inakuwa faulo.
Dak ya 26, timu zote zinaonekana kucheza kwa malengo.
Dak ya 24, anapiga Abdul mwenyewe, piga pale, inatokea piga nikupige lakini kipa anapangua na Polisi wanaokoa, wanapiga mpira mbele.
Dak ya 23, Yassin Mustapha anapata kadi ya njano kwa kumchezea rafu Juma Abdul, inakuwa faulo, ni kulia mwa lango la Polisi, karibu kabisa na eneo la hatari.
Dak ya 22, Raymond anapiga shuti kali na linakwenda sentimita chache juu ya lango la Yanga, tungesema mengine.
Dak ya 21, namna gani Yanga wanafanya uzembe mwingine kwenye lango la Polisi, ingekuwa ni bao la pili.
Dak ya 19, Makame anapokea pasi katikati ya uwanja, anajaribu kusaka mchezaji wa kumpasia, piga mbele kule mpira unakuwa hauna macho, Polisi wananyakua.
Dak ya 18, Molinga anafanya matumizi mabaya ya mwili kwa kumhadaa mwenzake wa Polisi, inakuwa faulo.
Dak ya 17, Polisi wanaonekana kuwa na mipango licha ya kuwa nyuma kwa bao 1-0, namna ya kuipenya ngome ya Yanga ni ngumu.
Dak ya 16, Golikiki, mpira unaelekezwa Yanga, ni baada ya Nchimbi kuutoa.
Dak ya 15, Balinya sasa na mpira, anajaribu kupenyeza pasi kati mwa uwanja, mpira unakataa.
Dak ya 14, Nchimbi anaonekana anaonekana akiwa anatoa maelekezo kwa wenzake, ni juu ya kuhakikisha wasawazisha bao.
Dak ya 13, Ngassa anapandisha mashambulizi mbele, anarejesha nyuma wanaanza tena upya Yanga.
Dak ya 12, Sixtus Sabilo amepata nafasi ya kutengeneza bao kwa Polisi lakini amekosa umakini.
Dak ya 11, faulo inapigwa kuelekezwa Yanga, ni baada ya kutokea madhambi.
Dak ya 10, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera anaonekana akiwa jukwaani akiitazam mechi vizuri.
Dak ya 6, Ngasa anipatia Yanga bao la kwanza kufuatia krosi safi kulia mwa uwanja iliyopigwa na Juma Abdul.
Dak ya 03, mpira umetoka, Yanga wanarusha, ni kuelekea lango la Polisi.
Dak ya 2, Polisi Tanzania wanashafanya shambulizi la kwanza, wanakosa, kipa Mnata anadaka.
Dak ya 1, mechi imeshaanza.
Kupoteza pointi 6 ni nyingi mnooo, huyu Zahera namna gani?
ReplyDeleteEti badoo vyura ni wa kimataifa! Yule kipa wa Polisi ni namba mbili..Bahati Yaounde wamechomoa
ReplyDeleteKwa Wapenzi wa Yanga tu
ReplyDeleteUongozi wa Dkt Msolla hausikilizi maoni ya wadau nimeuandikia e-mail nyingi mno kuwashauri na kuwakumbusha mambo ya msingi ili ushindi upatikane lakini WAMEYAPUUZA sasa nyinyi wenyewe mnashuhudia matokeo yake....waambieni waangalie email kutoka kwa Al Lec wazipitie na kuzifanyia kazi...
Benchi jipya la ufundi pamoja na uongozi mzima wa daktari Msola uko vizuri sana kwakweli naupongeza sana tuendelee kua wavumilivu kombe linarudi yanga hata mia ilianza na 0 ikaja 1....mpaka 1000....> nakuendelea.
ReplyDelete