Yanga ndiyo waliokuwa wa kwanza kuandika bao la mapema mnamo dakika ya 6 kupitia kwa Mrisho Ngassa baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa Juma Abdul aliyeipiga kulia mwa uwanja.
Polisi walijibu mapigo mnamo dakika ya 34 kipindi cha kwanza kupitia kwa Ditram Nchimbi aliyeingia kambani mara tatu leo.
Mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika, Yanga na Polisi wakuwa sawa kwa matokeo ya 1-1.
Mnamo kipindi cha pili Polisi walikuja juu na kuandika bao la pili kupitia kwa yuleyule Nchimbi aliyefunga baada ya kupokea pasi safi iliyopenyezwa katikati mwa uwanja kumfunga kiufundi kipa Metacha Mnata ikiwa ni dakika ya 55.
Na katika dakika ya 58 tena, Nchimbi aliingia tena kambani akifunga mpira wa kichwa na kufanya matokeo yawe 3-1.
Yanga waliamka tena kwa kasi ya ajabu ambapo David Molinga 'Falcao' alifunga katika dakika ya 65 baada ya kipa wa Polisi, Kulwa Manzi kushindwa kuumiliki mpira vizuri baada ya kumponyoka na kuelekea nyavuni.
Mnamo dakika ya 69 tena, Molinga aliingia tena kambani kupitia mpira wa faulo ambao ulimzidi nguvu kipa wa Polisi, na mpaka kipyenga kinamalizika, matokeo ni 3-3.
Wachezaji wetu wamechoka au? Kocha alitakiwa kuwapa na fasi wale ambao hawakucheza Zambia na Dar es Salaam ilipokutana na Zesco, Akina Mustafa, Jaffary, Birigimana nk. aache kukariri!
ReplyDeleteKwa Wapenzi wa Yanga tu
ReplyDeleteUongozi wa Dkt Msolla hausikilizi maoni ya wadau nimeuandikia e-mail nyingi mno kuwashauri na kuwakumbusha mambo ya msingi ili ushindi upatikane lakini WAMEYAPUUZA sasa nyinyi wenyewe mnashuhudia matokeo yake....waambieni waangalie email kutoka kwa Al Lec wazipitie na kuzifanyia kazi...
Watani wasingechezeshwa kindumbwendumbwe na timu mpya ingekuwa Zahera hkupigwa marufuku kukaa bao la ufundi lakini cha muhimu Molinga katia bao
ReplyDeleteRudi Nyumbani Kume Noga
ReplyDeleteSaleh Jembe Naomba Utuletee Msimamo Wa Ligi Tuone !
Siku zote namba huanza na 0,1,,,,,
DeleteKelele za vyura zitakwisha tu.
ReplyDeleteKwa Wapenzi Wa Yanga Wanaoumia Tu
ReplyDeleteUongozi Wa Dkt Msolla Hausikilizi Maoni Ya Wadau Nimeuandikia E-Mail Nyingi Mno Kuwashauri Na Kuwakumbusha Mambo Ya Msingi Ili Ushindi Upatikane Lakini WAMEYAPUUZA Sasa Nyinyi Wenyewe Mnashuhudia Matokeo Yake....Waambieni Waangalie Email Kutoka Kwa Al Lec Wazipitie Na Kuzifanyia Kazi...
Leo Zahera alitamka na kuahidi kuwa kazi inaanza Leo na khushinda mechi za ligi zote zinazokuja tena Kwa idadi kubwa sana ya magoli na tuliyoshuhudia leo ndio mwanzo wa safariv
ReplyDeletePolisi ndiyo imelazimishwa sare. Not the other way round.
ReplyDeleteVaada ya mchezaji wao mmoja kupewa nyekundu na kuendelea na wachezaji kumi na watani kuwa na wachezaji kamili
ReplyDeleteHiyo ndio yanga ya kimataifa.mpaka ipunguziwe maadui ndio inashinda vita,wangeandamana goli la makame iweje wapewe zesco?
ReplyDeleteLabda ndiomana wanaendelea kujiita wakimataifa.
ReplyDeletePOVU RUKSAAAAAAAA.
ReplyDelete