MAN UNITED KUSHUKA DARAJA MSIMU HUU, NYINGINE KALI ZA LEO ULAYA HIZI HAPA
Kuna uwezekano Manchester United ikashuka daraja msimu huu, kwa mujibu wa kocha wa zamani wa England, Sam Allardyce. (Talksport)
Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer atafutwa kazi endapo timu yake itafungwa na Norwich mwishoni mwa mwezi, ripoti zinaeleza. (Sun)
Hata hivyo, vyanzo vingine vinaarifu kuwa uongozi Man United upo tayari kumvumilia na kumpa muda zaidi Solskjaer wa kufanya mageuzi klabuni, licha ya kiwango kibovu cha matokeo ya mwanzo wa msimu kwa miaka 30. (Telegraph)
United wanapanga kuwasajili kiungo wa West Ham na England Declan Rice, 20, na beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28, bila kujali mustakabali wa Solskjaer. (Goal)
Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino napanga kuwauza wachezaji kadhaa wa klabu hiyo baada ya kuanza msimu kwa kiwango kibovu. Wachezaji watakaowekwa sokoni mwezi Januari ni; Eric Dier, 25, Christian Eriksen, 27, Serge Aurier, 26, Victor Wanyama, 28, pamoja na Danny Rose, 29. (Times - subscription required)
Kocha David Moyes yupo tayari kurudi kuifunza klabu yake ya zamani ya Everton, katika kipindi ambaco kocha wa sasa Marco Silva akiwa katika shinikizo kubwa baada ya timu hiyo kuwa chini ya mstari wa kushuka daraja. (Mirror)
Crystal Palace watalazimika kulipa pauni milioni ili 22 wamsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Michy Batshuayi, 26, ambaye yupo kwa mkopo Palace toka Januari mwaka huu. (Express)
0 COMMENTS:
Post a Comment