October 9, 2019


LIGI ya Saud Arabia ni miongoni wa Ligi ghali ambazo zinatumia gharama kubwa kwenye uendeshaji wake Jambo lililowafanya wakubali kutumia teknolojia ya VAR ili kuendana na ubora mabadiliko ya FIFA.

Mapokeo ya teknolojia hiyo yamekuwa na changamoto kwani kwenye mchezo kati ya Al-Nassr na Al-Fateh VAR ilishindwa kutumika vema kutokana na ukorofi wa waendeshaji mitambo.

Fernando Trisaco, Rais wa Kamati ya Marefa alipewa ripoti iliyoeleza kilichotokea kwenye mchezo huo baada ya kuhoji: 
"Mnapaswa mtueleze ukweli nini kilitokea, mwanzo kila kitu kilikuwa sawa Ila ghafla mambo kwenye VAR yakakata vyumba vyote kwa nini, sababu ni ipi?," Alihoji.

Jibu alilopewa ni kwamba kuna mfanyakazi alichomoa waya uliokuwa ukitoa taarifa za VAR na kuweka simu yake chaji Jambo lililofanya kusiwe na mawasiliano tena Kwenye teknolojia hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic