October 1, 2019


Mshindi wa tuzo ya muziki ya Grammy kwa muziki wa reggae, Louie Rankin, aliyepata umaarufu kwa kufanya kazi na nyota kama DJ Khalid na DMX, amefariki jana, Septemba 30, kwa ajali ya gari iliyohusisha pia lori la mizigo.

Msanii huyo alizaliwa Kingston, Jamaica, na alipata umaarufu sana katika igizo la filamu ya Belly akijulikana kama Ox mwaka 1998 aliposhirikiana na waigizaji wengine, Nas na DMX.

Rankin alipata tuzo ya Grammy mwaka 1992 kwa wimbo wake wa  ‘Typewriter’ na kuigiza katika filamu za Shottas, mwaka 2002, na  We Run These Streets,  mwaka 2014.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic