October 8, 2019


Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema kuwa hali yake si shwari tena kutokana na kusumbuliwa na macho.

Akilimali ambaye hivi karibuni alienda hospitalikwa ajili ya vipimo kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa kisukari, ameanza kusumbuliwa na macho ambayo yamepelekea asione vizuri.

Ameeleza haoni vema na akisema amejitahidi kuzungumza na viongozi wake wa Yanga lakini hawajampa ushirikiano wowote.

Amefunguka kuwa alienda kunako makao makuu ya klabu kwa usafiri wa Bajaji na akamtafuta kiongozi mmoja wa juu pale Yanga lakini hakuonekana kumsaidia.

Ni mwezi takribani wa pili sasa au zaidi Akilimali amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo ambao umepelekea hivi sasa asione vema.

"Ninasumbuliwa na macho, sioni vuziru kwa sasa.

"Nimejitahidi kuwasiliana na viongozi wenzangu Yanga lakini hamna walichonisaidia chochote.

4 COMMENTS:

  1. Mzee amesababisha Yanga kuwa ombaomba sasa nani atakayempatia msaada?Mi namshauri aende Simba waliomtuma kuichanganya Yanga wanaweza kumpa hata elfo 50.

    ReplyDelete
  2. wachezaji wengine wanadai mshiko hv watamkumbuka mzee wawatu kweli

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic