Mkuu wa Huduma kwa wateja wa MultiChoice Tanzania Ngwitika Mwakihesya (kushoto) na Afisa Uhusiano Diana Ayo wakiwa na baadhi ya watoto waliofika na wazazi wao katika tawi la DStv Mlimani City mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali. MultiChoice inaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo pamoja na mambo mengine, itatoa zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi na wateja wake ikiwemo pia kuwatembelea wateja na kukusanya maoni yao ili kuweza kuboresha zaidi huduma zake. |
Kampuni ya MultiChoice Tanzania imeanza maadhimisho ya wiki ya wateja ambapo itaendesha shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa zawadi kwa wafanyakazi na wateja kwa muda wa mwezi mzima.
Mkuu wa huduma kwa wateja Ngwitika Mwakihesya amesema kuwa katika kipindi hicho, MultiChoice Tanzania itakuwa na matukio mbalimbali yenye lengo la kuiwezesha kuwasogelea wateja karibu zaidi na kufahamu kwa kina uzoefu wao wa kupata huduma za DStv.
‘MultiChoice inaamini kuwa wafanyakazi na wateja wetu ndiyo nguzo ya ustawi wetu hivyo katika kipindi hiki tutahakikisha tunawafikia na kuwasikiliza maoni yao na hili tunalifanya ili tuweze kuboresha zaidi huduma zetu na kumfanya mteja ajisikie kuwa yeye kweli ni mfalme,” alisema Ngwitika na kuongeza kuwa zoezi hilo litahusisha kuwazawadia wafanyakazi mbalimbali pamoja na wateja na pia kuwatembelea wateja wao maeneo mbalimblai ili kuwasikiliza na kupata maoni yao.
Mkuu wa Huduma kwa Wateja wa MultiChoice Tanzania Ngwitika Mwakihesya akimuelekeza mmoja wa wateja waliofika katika tawi la MultiChoice Mlimani City Aziz Makupa jinsi ya kupata huduma mbalimbali za DStv ikiwa ni sehemu ya maaadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Kushoto ni afisa wa huduma kwa wateja wa tawi hilo Vedastina Ishengoma. Katika maadhimisho hayo, MultiChoice itatoa zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi na wateja wake ikiwemo pia kuwatembelea wateja na kukusanya maoni yao ili kuweza kuboresha zaidi huduma zake.
|
Amesisitiza kuwa kutokana na uzito huo, zoezi la kutembelea wateja litafanywa kwa kushirikiana na uogozi wa kampuni hiyo “Zoezi hili la kuwatembelea wateja litafanywa kwa kushirikiana na viongozi hivyo hata mkurugenzi mwenyewe na timu yake ya Menejimenti wataenda kuwatembelea wateja” alisisitiza Ngwitika.
0 COMMENTS:
Post a Comment