SELEMAN Matola, Kocha
wa Polisi Tanzania amesema kuwa kwa sasa hasira zake za kupoteza mchezo wake wa
kwanza mbele ya Ruvu Shooting zinaelekea kwa Yanga.
Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa anatambua ugumu wa kupambana na timu ya
Yanga kutokana na mabadiliko waliyoyafanya ila hesabu zake ni pointi tatu.
“Natambua kwamba Yanga
imetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na ina hasira ya kupoteza isisahau
kwamba nasi tumepoteza mchezo wetu wa kwanza mbele ya Ruvu Shooting tena kwa
kujifunga wenyewe bahati mbaya na tuliwadhibiti wapinzani wetu.
“Maandalizi yetu yapo
sawa na dozi kwa vijana inaendelea, historia yangu ya kushinda mbele ya Yanga
hiyo naachana nayo kwani mpira hatuzungumzii wakati uliopita tunazungumzia
dakika tisini, mashabiki watupe sapoti,” amesema.
Polisi Tanzania
inatarajia kucheza na Yanga, kesho, Uwanja wa Uhuru, ina pointi
tatu ilizozibeba mbele ya Coastal Union kwenye uwanja wa Ushirika.
0 COMMENTS:
Post a Comment