HALI inazidi kuwa moto ndani ya Singida United baada ya kupigwa chini kwa aliyekuwa Kocha Mkuu Felix
Minziro mpaka sasa imetumia dakika 450 kusaka pointi mbili pekee.
Singida United imecheza
jumla ya michezo mitano ndani ya Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na Vodacom
haijapata ushindi kwenye michezo hiyo zaidi ya kuambulia sare pekee.
Ilianza kupoteza mbele
ya Mwadui FC kwa kufungwa bao 1-0, ikapoteza mbele ya Namungo FC kwa kufungwa
mabao 2-0,ikalazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Ndanda FC pia ikalazimisha
sare ya 0-0 na Mbao FC kabla ya kupoteza mbele ya Alliance kwa kufungwa bao
1-0.
Kwenye michezo mitano
iliyocheza mpaka sasa imefunga jumla ya bao 1 na imefungwa mabao matano yanayoipa
pointi mbili.
0 COMMENTS:
Post a Comment