STRAIKA MBRAZIL SIMBA AINGIA VITANI NA KAGERE, ATAJA IDADI YA MABAO ATAKAYOFUNGA
Straika mpya wa Simba kutoka Brazil Wilker Da Silva, amesema kama atapewa nafasi ya kucheza msimu huu anaweza kumalizi ligi akiwa ameingia kambani mara 15.
Wilker ambaye tangu asajiliwe msimu huu, amecheza mechi moja ya ligi ambayo ilikuwa ni dhidi ya Kagera Sugar akiingia kutokea benchi kipindi cha pili.
Wilker ameeleza kuwa baada ya kuanza mazoezi, Kocha Patrick Aussems alimwamini haraka na kumpanga katika mechi dhidi ya Kagera ingawa hakucheza muda mrefu.
Alieleza ndani ya kikosi cha Simba kuna wachezaji wengi wenye vipaji hivyo kwake inamtaka muda mrefu kuzoea na anaamini ataonesha kiwango kizuri.
"Sijafunga bao hata moja, lakini kama nikiendelea kuwa vizuri na nikiendelea kupata nafasi kwa kushirikiana na wenzangu naweza kufunga mabao 10 mpaka 15.
"Kikosi cha Simba kipo vizuri, hivyo naweza kusema nitazidi kupambana ili kutomwangusha Kocha wangu kadri atakapokuwa ananipa muda."
0 COMMENTS:
Post a Comment