October 4, 2019


Ni kama utani vile, unaambiwa nyota ya straika hatari wa Simba, Meddie Kagere inazidi kung'ara baada ya kupata dili jingine kutoka Marekani.

Taarifa kwa mujibu wa Meneja wa Kagere, Patrick Gakumba, ameibuka na kusema kwa kasi aliyonayo, tayari ameshamuandalia ofa nzuri katika klabu ya Dallas FC iliyopo Texas, Marekani.

Gakumba ameibuka na kusema moja kati ya masharti ambayo Dallas wanayataka ili Kagere wamchukue ni kuhakikisha anafikisha mabao 25 msimu huu kunako Ligi Kuu Bara,

“Najua kwa sasa Kagere ni mali ya Simba, nawasiliana naye nikimtaka azidi kuitumikia klabu hiyo kwa nguvu zote huku akikumbuka deni la mabao 25 linalohitajika.

"Dau la kule litakuwa ni nono zaidi ya Msimbazi, na tayari jina lake limeshajulikana katika nchi nyingi za Afrika na duniani kwa ujumla."

Mpaka sasa Kagere aliyecheza mechi nne msimu huu ameingia kambani mara sita huku wachezaji wanaofuatia ni Miraji Athumani na Ditram Nchimbi walio na mabao matatu kila mmoja.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic