WAWA APEWA WAKATI MGUMU SIMBA
Beki wa Simba Muivory Coastal, Pascal Serge Wawa amesema changamoto kubwa anayokutana nayo ni mawasiliano kati yake na Wabrazil, Tairone Santos da Silva, Fraga Gerson na Wilker dos Santos.
Wabrazil hao walijiunga na Simba kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara kwa ajili ya kukiimarisha kikosi hicho. Tairone anacheza nafasi ya beki wa kati pamoja na Wawa na Fraga yeye ni kiungo mkabaji anayemudu kucheza namba sita.
Wawa amesifu viwango vya wachezaji hao licha ya kukabiliwa na changamoto hiyo ya lugha ambao hawajui Kifaransa, Kingereza na Kiswahili.
Wawa alisema ni shida kwake yeye na wenzake huku akiamini siku chache zijazo wataongea vizuri Kiingereza na Kiswahili.
Aliongeza kuwa, wanaelewana kidogo vizuri wanapokuwa uwanjani kutokana na lugha ya mpira kujulikana, lakini nje ya uwanja ni shida.
“Kwa Fraga yeye hana shida kabisa, kwani anaelewa Kiingereza hivyo inakuwa rahisi kwangu kuzungumza na wachezaji karibia wote,”alisema Wawa.
Wawa aliongeza; “Muda wangu mwingi natumia kufanya mazoezi bila kutumwa na mtu sababu napenda kile ambacho ninakifanya ndiyo maana utaona nipo gmy au nakimbia na mazoezi ya aina nyingine na hii ni kuwa bora zaidi uwanjani.
“ Kama unavyofahamu soka ni ushindani na huwezi kupambana bila kujipanga ni jambo la msingi sana kujituma na kuweka malengo hasa kile unachokifanya mazoezi ndiyo kila kitu kwa mchezaji yeyote hata kama unakipaji ndiyo siri ya mafanikio yangu.
Hata hivyo, Wawa aliongeza kuwa hata kipindi cha mapumziko anafanya mambo yake binafsi bila kusahau kufanya mazoezi sababu anajua umuhimu wake.
Katika mechi nne ambazo Simba imecheza msimu huu safu yake ya ulinzi imeruhusu mabao mawili tu na mabeki waliofanya kazi hiyo Wawa ni mmoja wapo.
0 COMMENTS:
Post a Comment