October 1, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amefunguka kwa kusema lawama zote anazibeba yeye baada ya kupoteza mechi ya raundi ya pili dhidi ya Zesco United.

Yanga ilipoteza mchezo wa juzi Jumamosi kwa kipigo cha mabao 2-1 na kuwaondoa moja kwa moja katika michuano hiyo ambapo sasa watacheza shirikisho.

Kutokana na kipigo hicho, Zahera amesema anastahili lawama ziende kwake sababu ya kuchelewesha kufanya mabadiliko kutokana na wachezaji kuwa kwenye mipango yake.

Zahera alieleza kuwa hakufanya mabadiliko haswa kwa Abdulaziz Makame ambaye alijifunga sababu alihitaji kumtumia kwenye upigaji penati.

"Sikufanya mabadiliko kutokana na wachezaji kuwa kwenye mipango yangu.

"Makame ambaye alijifunga sikumtoa sababu nilitegemea mechi ingeenda mpaka hatua ya matuta namimi nilimuacha Makame sababu ni mpigaji mzuri."

4 COMMENTS:

  1. Gharama ya Makosa ya Kiufundi kwa upande wa Mwalimu ni makubwa na yanaleta madhara kwa mfano wadau wanapewa rungu la sababu kujenga hoja ya kusema Kocha hafai na hivyo atimuliwe....wapenzi wa soka wa Tanzania sio wavumilivu na hawapendi kuvuta subira kwa makocha wanaokiri madhaifu yao kama anavyofanya Zahera....sasa unaamsha fikra kuwa usemi ule kwamba Kocha aondolewe uko sahihi....Sidhani ni picha nzuri kusema kama mwalimu mimi ndiyo nastahili lawama kwenye kadhia ya uma wa wanaozisoma habari hizi.

    ReplyDelete
  2. Kwanini aondolewe. Kosa moja haliwachi mke. Samaki akioza usimtupe, umtafutie viungo umkaushe, atamuokota mwenzio ulie uje ujute

    ReplyDelete
  3. Mtani hakuna haja ya kulalama jitayarishe kwa Seleman Matola

    ReplyDelete
  4. Hivi hiyo timu yenye usajili wa wachezaji takribani wote wapya mlitegemea ifanye maajabu yapi katika mashindano ya kimataifa ambayo timu haikuyatarajia? Tatizo letu ni kujisahaulisha kwamba hiyo timu ilipata lifti michuano ya kimataifa huku pia tukijisahaulisha kwamba hata Azam na KMC waliojiandaa mapema nini kimewakuta.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic