ZAHERA AWATAJA WACHEZAJI WALIOSABABISHA YANGA ITOLEWE NA ZESCO
Baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Zesco katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi iliyopita, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema endapo angefanya mabadiliko, matokeo yasingekuwa 2-1.
Kauli ya Zahera imekuja kufuatia kutofanya mabadiliko baada ya kuweka wazi kuwa wachezaji wake walikuwa kwenye mipango yake.
Zahera alisema alichelewesha kufanya mabadiliko akiamini mechi ingemalizika kwa sare ya 1-1 na wangeweze kufikia hatua ya kupiga matuta.
Lakini Zahera ameibuka na kusema kama angefanya mabadiliko mapema haswa kuwatoa Abdulaziz Makame na Feisal Salum 'Toto' ambao aliona wamechoka, matokeo yangekuwa mengine.
"Kama ningefanya mabadiliko mapema ya Toto na Makame waliokuwa wamechoka katika safu ya kiungo ya timu yangu, matokeo yasingekuwa hivyo.
"Nipende tu kuwapongeza wachezaji wangu kwa kupambana vizuri na sasa tunaelekeza nguvu zetu zote kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho."
Mabadiliko hayo yangeimaliza kabisa Yanga pale katikati ni bora hakufanya hivyo....
ReplyDeleteKichwa cha Habari mara nyingine kinaleta lugha tata yenye hulka ya uchonganishi na yenye asili ya negativity
ReplyDeleteMUANDISHI KUA MAKINI NA UANDISHI WAKO,NDIO MAANA SERIKALI INATAKA MKASOME
ReplyDeleteMdau nakuunga mkono kabisa , maana kicha cha habari na habari yenyewe ni dhahiri uchochezi au unazi
DeleteHalafu wanaanza na baada ya kupoteza kwa bao 1-0 na Zesco .wakati walifungwa 2-1 hao ndio waandishi wetu makanjanja.
ReplyDelete