UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kwa sasa mipango yao ni kuona wanabeba pointi tatu muhimu mbele ya Singida United kwenye mchezo utakaochezwa Jumatano, Jnauri mMosi 2020.
Azam FC iliyochini ya Arstica Cioaba ilishinda mbele Polisi Tanzania kwa bao 1-0 lililofungwa na Obrey Chirwa dakika ya tisa.
Ofisa Habari wa Azam FC, amesema kuwa wamejipanga kufanya vema kwenye mechi yao dhidi ya Singida United utakaochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
"Tumeanza kuivutia kasi Singida United na tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila tutapambana kupata pointi tatu, tayari benchi la ufundi limeanza kusimamia mazoezi na mipango kuhusu mechi yetu, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment