MSHAMBULIAJI wa Everton, Dominic Calvert-Lewin amewekwa kwenye rada za uongozi wa Manchester United ili ajiunge kwenye usajili wa mwezi Januari, 2020.
United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer inaelezwa kuwa inamtaka nyota huyo aongeze nguvu ndani ya United baada ya kumkosa Erling Haalad aliyejiunga na Borussia Dortmund.
Imeripotiwa kuwa dau la nyota huyo ni pauni Milioni 50 jambo linalowapasua kichwa United kuziweka mezani kwa sasa ili kuipata saini yake.
Dominic Calvert-Lewin mwenye umri wa miaka 22 ametupia jumla ya mabao 10 kwenye michuano yake yote ya ushindani akiwa amecheza jumla ya mechi 22.
0 COMMENTS:
Post a Comment