UONGOZI wa
KMC um ewataka mashabiki wao wasiwe na hofu na mlinda mlango wao namba moja Juma
Kaseja ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti hivi karibuni.
Kaseja
aliyejiunga na KMC msimu wa mwaka 2018-19 ilipokuwa chini ya Etienne
Ndayiragije kutoka Kagera Sugar aliukosa mchezo dhidi ya Simba ambao KMC
walipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 uwanja wa Uhuru kutokana na kuwa majeruhi.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa kwa sasa
maendeleo ya Kaseja yanaridhishwa hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi.
“Kwa sasa
maendeleo ya Kaseja sio mabaya kwani ameanza kurejea kwenye ubora wake taratibu
kabla ya kuungana na wachezaji wenzake kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
0 COMMENTS:
Post a Comment