KOCHA Mkuu wa Namungo FC, Hitimana Thiery amesema kuwa timu yake inajiandaa kumnasa mshambuliaji mpya raia wa Uganda kwa ajili ya kuimarisha eneo la ushambuliaji.
Katika kipindi hiki cha dirisha dogo la
usajili, timu nyingi hufanya mabadiliko ili kuimarisha vikosi vyao na
ndiyo hali ilivyo kwa kocha wa Namungo FC.
Hitimana amesema kuwa kwa sasa uongozi wa timu hiyo upo
kwenye mazungumzo na mshambuliaji uraia wa Uganda ambaye
hapo awali alicheza katika Ligi Kuu ya nchini Congo.
“Kiukweli
kwa sasa tupo kwenye mazungumzo na mshambuliaji mmoja ambaye aliwahi
kucheza Ligi ya nchini Congo na mazungumzo yanaenda vizuri, kwa hiyo
muda wowote tukimalizana nae tutawaambia,” amesema Hitimana.
0 COMMENTS:
Post a Comment