December 30, 2019


DAVID Molinga wengi wanapenda kumuita mwili jumba ama falcao mshambuliaji wa Yanga raia wa Congo guu lake la kulia limekwama uwanja wa CCM Kirumba kwa muda wa dakika 270 bila kucheka na nyavu ndani ya Ligi Kuu Bara.
Molinga mwenye mabao manne kwa sasa alianza kwa kasi ya kutupia huku akipata umaarufu kwa kutumia zaidi guu la kulia kufunga mabao ya moja kwa moja akiwa nayo mawili mpaka sasa akiwa.
Alianza kufunga bao lake la kwanza kwenye mchezo wa pili wa Yanga dhidi ya Polisi Tanzania kwenye sare ya mabao 3-3 ambapo alifunga dakika ya 64 kwa kichwa akimalizia pasi ya Mrisho Ngassa na la pili alifunga kwa faulo dakika  ya 68 kwa guu lake la kulia.
Bao la tatu alifunga mbele ya JKT Tanzania kwa faulo dakika ya 34 baada ya Deus Kaseke kuchezewa faulo  na  Yanga ilishinda mabao 3-2 dhidi ya JKT Tanzania mechi zote zilichezwa uwanja wa Uhuru.
Mara ya mwisho kufunga bao lake la nne ilikuwa uwanja wa CCM Kirumba ambapo guu lake la kulia lilicheka na nyavu dakika 71 akimalizia pasi ya Deus Kaseke kwenye ushindi wa mabao 2-1 na hakuweza kufurukuta kwenye mechi tatu za Yanga ambazo ni sawa na dakika 270 akiwa uwanjani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic