Baada ya Azam kusema kuwa imemalizana na klabu ya Yanga kuhusu Mshambuliaji Ditram Nchimbi, usajili wa mshambuliaji huyo umechukua sura mpya baada ya klabu yake anayoichezea kwa mkopo ya Polisi Tanzania kusema kuwa bado inamtambua Nchimbi kama mchezaji wao mpaka msimu wa 2019/2020 utakapomalizika.
Kaimu Katibu Mkuu na Afisa habari wa Klabu hiyo Frank Lukwaro akizingumza na gazeti hili amesema Azam waliwapa mchezaji huyo kwa mkopo wa mwaka mmoja hivyo suala la wao kumalizana na Yanga ni hatua moja hivyo Yanga wanapaswa kuja mezani kwa ajili ya kumalizana na Polisi Tanzania kwakuwa bado ni mtumishi wao kwa mujibu wa taratibu za usajili wa mchezaji kwa njia ya mkopo (Loan Transfers) zilizomleta kucheza ndani ya Vijana hao ambao makazi yao ni Shule ya Polisi Tanzania zamani Ikijulikana kama CCP mkoani Kilimanjaro.
"Huyu ni mchezaji wetu kwa sasa pamoja na kwamba alikuwa mali ya azam lakini sisi ndio mabosi wake kwa sasa na hata Azam wiki iliyopota walimuomba arudi kwao kabla ya msimu tukakataa kwakuwa hayakuwa makubaliano yetu ya awali yaliyomleta kwetu ambayo yanasema atacheza kwa msimu mzima na sasa msimu bado haujaisha.
"Kilichopo ni dirisha dogo ambapo kama wanahitaji huduma yake na sisi tunapaswa kushirikishwa kwa sababu tulishamuweka katika mipango yetu " Alisema Lukwaro.
Alisema baada ya kusikia azam wamemtangaza Nchimbi kuwa ni mali ya Yanga kwa sasa wanawasubiri Yanga mezani ili waweze kumalizana nao na hakuna ujanja kwakuwa wao ndio wenye uhalali.
Aidha, Lukwaro alisema wao hawawezi kumbania mchezaji yeyote kwenda klabu anayoitaka ispokuwa wanachohitaji ni taratibu kufuatwa ambapo aliongeza kuwa katika wamewekeza mambo mengi mpaka Nchimbi kurudia makali yake hivyo ni lazima Azam na Yanga wawaheshimu
Wameingizwa chakani mchana kweupe
ReplyDeleteHakuna kinachoshindikana hapo anaeozesha motto ni mwenye mtoto sio njomba
ReplyDeleteEndeleeni kuleta janja kwenye usajili mwisho mchezaji anakuja kukaa benchi mwaka mzima.
ReplyDeleteHuyu jamaa angejifanyia tathmin unajua,myself naona bora angekwenda kmc au namungo angeonekana zaidi hata ya pale alipo,huko anakokwenda namhurumia sana but the time will tell.
ReplyDeleteZahera na wengineo wavute subira hela ikibakia baada ya kulipa wachezaji wapya ndio watafikiriwa wengineo kulipwa japo kwa vipindi
ReplyDeleteHao polisi wanaweweseka tu, mtendaji mkuu wa Azam ashalitolea ufafanuzi ilo suala na inavyoonekana kanuni zinawapiga chenga polisi Tanzania,mchezaji awezi kuwa na mikataba miwili kwa wakati mmoja, mmiliki halali wa mchezaji Ni Azam na sio polisi,kule amepelekwa kwa mkopo na akuna kipengele Wala makubaliano yeyote yaliyowekwa wakati wanamchukua kwa mkopo kwamba wakimuitaji kumrudisha au kumuuza wailipe polisi!! Polisi wanapoteza Mda tu kwnye suala ambalo liko wazi, na bado walielezwa na Azam Kama wanamtaka mchezaji kuendelea nae watoe mil,30 kwa sababu wamepata ofa, polisi walishindwa kuipata iyo pesa wakaiambia Azam iendelee na utaratibu mwingine wao walikuwa wanategea amalize mkataba mwezi wa 6 wampate bure sasa Azam nao walishtuka mapema wakausoma mchezo kwamba awatopata chochote wakafanya biashara, sasa kisheria na kikanuni Azam wako sahihi,akuna makubaliano yoyote ya kimaandishi yaliyowekwa wakati wanapeana mchezaji so polisi imekula kwao na liwe funzo kwa vilabu vingine vinapotoa mchezaji kwa mkopo kwenda klabu kingine lazima yawepo makubaliano ya kimaandishi ili kuondoa utata Kama huu!
ReplyDelete