UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa hesabu zao ni kupambana kutetea taji lao la kombe la Mapinduzi ambalo lipo mikononi mwao.
Michuano ya Mapinduzi inatarajiwa kuanza kutimu vumbi kuanzia Januari 5 hadi 13 2020.
Jaffary Maganga, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kikosi kimeanza maandalizi kwa ajili ya mechi zote zinazowahusu.
Mabingwa hao watetezi wa michuano ya Kombe la Mapinduzi wamepangwa kundi A likiwa na timu nyingine za Yanga, Jamhuri ya Pemba na Mlandege.
0 COMMENTS:
Post a Comment