December 23, 2019


NYOTA wa Simba, Ibrahim Ajibu ameweka rekodi ya kipekee kwa washambuliaji wazawa Tanzania wanaokipiga kwenye timu za Yanga na Simba kucheka na nyavu. 

Kwenye jumla ya mechi mbili ambazo wamecheza Simba na Yanga jumla ya mabao 10 yamefungwa huku tisa yakifungwa na wageni na moja tu likifungwa na Ajibu ambaye ni mzawa.

Yanga ilianza kushinda mchezo wake wa kwanza wa kombe la Shirikisho dhidi ya Iringa United Desemba 21 kwa mabao 4-0 uwanja wa Uhuru ambapo mabao yote yalifungwa na wageni.

Nahodha Papy Tshishimbi raia wa Congo, Lamine Moro raia wa Ghana, Patrick Sibomana raia wa Rwanda na David Molinga raia wa Congo ndio waliocheka na nyavu wote wakiwa ni washambuliaji wa kigeni.

Watani zao wa jadi Simba walishinda mabao 6-0 dhidi ya Arusha United jana Desemba 22Iliinyoosha Arusha United wafungaji wakiwa ni Gerson Fraga raia wa Brazili, Deo Kanda raia wa Congo, Francis Kahata raia wa Kenya, Clatous Chama raia wa Zambia, Meddie Kagere raia wa Rwanda huku Ibrahimu Ajibu akiwa mzawa pekee aliyefunga bao katika mabao 10 yaliyofungwa na timu hizi zenye ushindani Bongo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic