UONGOZI wa KMC umesema kuwa kwa sasa bado mambo ni magumu kwao kumpata mshambuliaji wa Simba Rashid Juma ili aungane na kikosi chao kutokana na kutopewa ripoti ya kocha.
KMC inaelezwa kuwa ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na Juma ambaye hana nafasi ya kudumu ndani ya kikosi cha Simba kutokana na ushindani wa namba na inamtaka kwa mkopo ili aongeze uzoefu.
Habari kutoka ndani ya KMC zimeeleza kuwa uhitaji wa kusajili nafasi ya mshambuliaji ni kubwa ila ripoti ndiyo inachelewesha mambo ndani ya KMC kutokana na ratiba kuwabana.
"Nafasi moja tu ndiyo inahitajika kwa sasa ndani ya KMC na ni Juma ambaye yupo kwenye hesabu ila ugumu upo kwenye kukamilisha mpango huo kutokana na kucheleweshwa kwa ripoti pamoja na mechi ambazo zinabana," kilieleza chanzo hicho.
Kachukuweni huko yanga.
ReplyDeleteKachukuweni huko yanga.
ReplyDelete